Je,wajua mbu husherehekewa Urusi?

Image caption mbu

Watu wengi wanawachukia, lakini mbu sasa husherekewa kwa tamasha la kipekee katika mji mmoja huko Urusi.

Pengine la ajabu zaidi kwenye hafla hiyo ni kuwepo kwa mashindano ya kuchagua msichana mrembo zaidi, ambapo wasichana hao watahukumiwa kulingana na idadi ya alama za kuumwa na mbu baada ya kusimama kwa muda wa dakika 20 wakiwa wamevalia suruali fupi na fulana ndogo.

Haki miliki ya picha YOUTUBE BEREZNIKI TOWN
Image caption Tamasha la mbu Urusi

Jopo la majaji wataalamu wakiwepo madaktari wataikagua miili yao na mshindi atakua yule atakaye kuwa na alama nyingi za kuumwa na mbu, asema mratibu wa sherehe hiyo Natalya Paramonova.

Mwaka 2013, mshindi alikuwa na alama hizo za kuumwa na mbu mara 100.

Kwa wale wanao shangazwa na wazo hilo la kujitolea kuumwa na mbu hao, kuna mengine, shughuli ndogo ndogo zengine za ajabu zimezinduliwa ikiwepo shindano la kuona ni nani anayeweza kushika mbu aliye hai.