Kiongozi wa Taleban aunga mkono amani

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Mullah Omar

Kiogozi wa kundi la Taliban nchini Afghanistan Mullah Omar ameunga mkono mazungumzo ya amani na serikali.

Katika ujumbe usio wa kawaida kiongozi huyo wa Taliban anasema kuwa sheria ya kiislamu haizui kuwepo kwa mazungumzo ya amani na maadui.

Ameyataja mazungumzo hayo kama njia ya kumaliza kuwepo kwa majeshi ya kigeni nchini Afghanistan.

Licha ya Mullah Omar kutouzungumzia mkutano wa kwanza wa ana kwa ana na serikali ya Afghanistan ulioongozwa an Pakistan hayo ndio matamshi yake ya kwanza katika mpango huo wa amani.