Mawaziri wa fedha EU kuijadili Ugiriki

Haki miliki ya picha Getty
Image caption EU

Mawaziri wa fedha kutoka mataifa yanayotumia sarafu ya Yuro, wanajiandaa kuanza mkutano wa dharura, ili kujadili hatua itakayofuatia katika mazungumzo ya mzozo wa kifedha wa Ugiriki.

Mkutano huo ni wa tatu katika kipindi cha miaka mitano.

Katika kikao cha bunge cha usiku kucha, wabunge wa Ugiriki kwa kauli moja walipitisha masharti magumu ya msaada wa kifedha wa kuokoa uchumi wa taifa hilo, kama inavyotakikana na jumuia ya mataifa ya bara Ulaya - EU.

Waziri mkuu, Alexis Tsipras, amesema kuwa hana imani na masharti hayo, lakini hakuna njia nyingine kwa kuwa Ugiriki ingetaka kusalia ndani ya mataifa yanayotumia sarafu ya Euro.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bunge la Ugiriki

Spika wa bunge, Zoe Constantopoulou ameomba kupinga masharti hayo, huku akilaumu hatua hiyo na kusema ni usaliti wa viongozi.

Mbunge mmoja wa upinzani May Zanni, amesema kuwa masharti hayo ya IMF hayangetokea wakati huu mgumu.

Wabunge wengine walifyoka..., "Wewe ndiwe ulitufikisha hapa!" Naibu waziri wa fedha Nadia Valavani amejiuzulu, huku akisema kuwa hataweza kuunga mkono mipango hiyo.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kuongezwa kwa ushuru na mabadiliko katika sheria ya ajira.