Wabunge Ugiriki wakubali masharti magumu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption wabunge wa Ugiriki

Wabunge wa Ugiriki wamepitisha msaada wa kifedha wa kuokoa uchumi wa Umoja wa wenye masharti magumu.

Wakati wakipitisha mapendekezo ya msaada huo mapambano makali yalikuwa yakiendelea nje ya ukumbi wa bunge kati ya makundi yanaopinga mpango huo na polisi.

Yalikuwa ni mapambano makali kati ya polisi na waandamanaji nje ya ukumbi wa bunge. Wakati polisi walipokuwa wakipambana ndani ya ukumbi wa bunge hasira kali kutoka kwa baadhi ya wabunge wakati wa mjadala kabla wa kupitisha msaada huo wenye masharti magumu.

Waziri wa zamani wa fedha wa Ugiriki Yanis Varofakis amefananisha mpango huo na fidia wanayoitaka Ujerumani wakati mwisho wa vita vya kwanza vya dunia.

Yanis Varoufakis, m, in Greek: "Mwenye nguvu anataka walioshindwa kukubali masharti ambayo hawana haki ya kuwadai na walioshindwa wamekubali kutekeleza mambo ambayo hawana haki ya kutekeleza. Haya ni maneno ya John Maynard Keynes, katika mkataba wa Verlsailles. Tulichonacho mbele yetu ni mkataba mpya wa Versaille. Tupo kwenye kundi la nchi za Umoja wa Ulaya pamoja na Euclid ( Tsakalotos, Waziri wa Fedha) Tunapoondoka, tunapendekeza haki sawa, tunapendekeza mkataba halali, daraja ambalo tumepanga sawa na ule mpango wa Kansela wa Ujerumani, kumchagua Scheauble February 20." amesema Varoufakis

Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema haamini hatua zilizochukuliwa lakini kulikuwa hakuna jinsi kuupitisha msaada huo wenye masharti kwa Ugiriki inataka kubaki kwenye sarafu ya Euro.

''Naomba nikiri wazi kuwa masharti magumu haya ni magumu kwetu,na yana malengo ya manufaa binafsi, sikubaliano nayo, sina hakika kama ndiyo kuisaidia Ugiriki,na ni lazima tutekeleze masharti hayo.na hapo ndipo tunapotofautiana. Na kama ka namna yoyote ile mnaamini katika hali kama hii ,basi hapo naona hakuna namna nyingine zaidi ya sisi wote kukubali na kukabiliana na mzigo huu''. Amesema Tsipras.