Jeshi la Japan sasa kupigana nje

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Shinzo Abe bungeni

Bunge la uwakilishi la Japan, limeidhinisha kifungu cha sheria ya usalama yenye utata inayoleta mabadiliko inayoliruhusu jeshi la nchi hiyo kupigana katika mataifa ya kigeni tangu wakati wa kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.

Mabadiliko hayo ambayo yalipigiwa upatu na waziri mkuu Shinzo Abe, ambaye anasema kuwa itairuhusu Japan kukabiliana na vitisho hasa kutoka China.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeshi la Japan

Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni Hua Chunying, ameitaka Japan isalie katika njia ya maendeleo ya amani na kusaidia majirani zake.

Mabadiliko hayo yalianzishwa na waziri mkuu, Shinzo Abe, anayeamini kuwa ni muhimu kukabiliana na changamoto mpya inayoikabili Japan, hasa kutoka China.

Lakini wapinzani wanaamini kuwa marekebisho hayo, yanakiuka katiba ya Japan iliyobuniwa baada ya vita na inaweza kuyumbisha usalama wa taifa hilo, katika mzozo unaoongozwa na Marekani.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raia wa Japan wapinga sheria ya kuliruhusu taifa hilo kushiriki katika vita vya kimataifa

Baada ya hotuba kadhaa wakati wa mjadala huo bungeni, vyama vya upinzani vilikataa kuhudhuria shughuli za upigaji kura.

Kumeshuhudiwa upinzani mkali dhidi ya mabadiliko hayo, hali iliyosababisha kushuka kwa umaarufu wa bwana Abe.