Ufaransa yakwamisha shambulio la Kigaidi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve

Waziri wa Mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema vyombo vya usalama nchini humo vimefanikiwa kuwakamata watu wane wanaodaiwa kupanga njama za kushambulia maeneo ya jeshi.

Cazeneuve amesema kuwa watu hao walnaoshikiliwa miongoni mwao yupo mmoja aliwahi kuwa mwanajeshi mwenye umri wa miaka 30.

Idara za usalama nchini Ufaransa kwa sasa zimekuwa makini zaidi tangu kufanyika kwa mashambulizi yaliyosababisha mauaji ya watu 17katika mashambulizi yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Kiislam.