Samsung yazindua simu nyembamba zaidi

Haki miliki ya picha samsung
Image caption Samsung A8

Kampuni ya Samsung imezindua simu yake nyembamba zaidi aina ya smartphone kufikia sasa.

Simu hiyo kwa jina Galaxy A8 ina upana wa milimita 5.9 ikiwa ni wembamba wa asilimia 85 ikilinganishwa na simu ya Galaxy S6 Edge.

Licha ya wembamba huo waandisi wameweza kuiweka betri pamoja na kamera yenye uwezo wa mega pikseli 16.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Samsung Galaxy A8

Mmoja ya wataalam aliuliza swali la muhimu wa kutengeza simu nyembamba.

Kwa sasa Samsung imetangaza kwamba simu hiyo itauzwa nchini Uchina na Singapore.

''Galaxy A8 haitauzwa nchini Uingereza'' alisema msemaji wake.

Ijapokuwa itakuwa simu nyembamba zaidi kutoka kwa mojwapo ya kampuni kubwa ,kampuni nyengine za Uchina tayari zimeanza kuuza simu kama hizo.