Japan:Ujenzi wa uwanja wa Olimpiki wafutwa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Shinzo Abe

Japan inasema kuwa itafutilia mbali mpango mzima wa ujenzi wa uwanja mpya wa kitaifa wa michezo ya maandalizi ya mashindano ya Olimpiki mwaka 2020, na kuuanza upya.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Shinzo Abe, amewaambia wanahabari kuwa mradi huo unafaa uchunguzi mpya kwani unakumbwa na ukosoaji mkubwa kuhusiana na kiwango kikubwa cha pesa.

Kiwango cha hivi punde cha ujenzi wa uwanja huo wa Zaha Hadid ni dola bilioni mbili.

Unatazamiwa kuwa mwenyeji wa mchuano wa kombe la dunia la mpira wa raga mwaka 2019, lakini huenda usiwe umekamilika kufikia wakati huo.