Wanachama 6 wa Muslim Brotherhood wauawa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafuasi wa muslim Brotherhood

Watu sita wanaounga mkono kundi la Muslim Brotherhood wameuwawa katika makabiliano na raia mjini Cairo.

Kwa mjibu wa shirika la habari la MENA nchini Misri, makabiliano hayo yamefanyika leo Ijumaa.

Wizara ya usalama wa ndani imesema kuwa walinda usalama waliingilia kati ili kutuliza vurumai hilo na kuwatia mbaroni wanachama 15 wa Muslim Brotherhood.