Zaidi 40 wafa kwa milipuko Nigeria

Haki miliki ya picha BOKO HARAM
Image caption Wapiganaji wa Boko haram

Wafanyakazi wa uwokoaji Nigeria wanasema katika eno la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo katika mji wa Gombe watu arobaini wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya milipuko kutokea kwenye soko katika eneo hilo.

Mlipuko wa kwanza umetokea nje ya kwenye maegesho nje ya duka la viatu, na kufuatiwa na mlipuko mwingine muda mfupi baadae. Mmoja ya wafanyakazi wa uokoaji miongoni mwa waliouwa ni wanawake na watoto.

Mashuhuda wa tukio hilo amesema hali ni mbaya kwenye mitaa ya Gombe.

"Tulikuwa hapa sokoni na mara tukaona ndege inapaa angani na baadae ikapotolea mbali, ndani ya dakika tano tukasikia mlio mkubwa wa mlipuko. Tuliona watu wakilipuka kama matairi. Watu wengi walidhani ni matairi yamepasuka, na baadae sekunde chake tukawaona watu wameanguka chini wakiwa wameungua na kuanza kukimbia. Kulikuwa na mlipuko mwingine ambao nao umeua watu wengine. Tulijipa ujasiri na kuanza kuwaondoa watu na kuwapeleka hosptalini." Amesema Awalu Yakubu

Na shuhuda mwingine anasema alishuhudi vipande vya miili ya binadamu

"Kulikkuwa na vipande miiili ya binadamu kila mahali wakati tulipokuwa tukiwasaidia waliokuwa wamejeruhiwa. Mtu aliyeuawa kwenye duka lake aliwekwa kwenye begi, kumburutwa barabarani na kupakiwa kwenye gari. Na baadae majeruhi wakasafirishwa." Amesema shuhuda mwingine Haruna Abubakar