Obama kutozuru kijiji cha babaake Kenya

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Obama

#ObamainKenya ndilo neno linalotawala mitandao ya kijamii nchini Kenya huku rais huyo akitarajiwa kulitembelea taifa hilo.

Hatahivyo wakaazi wa kijiji cha Kogelo ambapo babaake Obama alizaliwa na kulelewa sasa hawatalazimika kufanya maandalizi ya aina yoyote kufuatia ziara hiyo baada ya balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec kusema kuwa rais huyo hatozuru kijiji cha Kogelo.

''Ana mda mchache sana kwa hivyo basi atakuwa nairobi pekee'',alisema bwana Godec akizungumza na runinga ya KTN.

Bibiye Obama Sarah Obama alikuwa amejiunga na wakaazi wa Kogelo akimtaka Obama kuwatembelea kulingana na ripoti za kituo cha habari cha Capital fm.