Wanajeshi 4 wauawa Marekani

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Barack Obama wa Marekani

Mtu mwenye silaha amewaua askari wanne wa jeshi la wana maji wa Marekani katika shambulio lililofanywa kwenye majengo mawili ya jeshi hilo katika mji wa Chattanooga, Tennessee.

Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo moja, Maafisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la ndani.

Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo, limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo.

Rais Obama ameyaelezea mazingira hayo kuwa ni ya kusikitisha kwa watu ambao wametumikia taifa kwa moyo wote na kisha kuuawa katika mfumo huu inasikitisha.

Naye Meya wa jiji la Chattanooga Andy Berke amesema muuaji wa wanajeshi hao aliuawa muda mfupi baada ya shambulio hilo. Pia ofisa wa polisi pamoja na watu wengine wamejeruhiwa.

Mwanasheria mkuu wa jimbo la Tennessee, Bill Kilden, ameyaelezea mauaji hayo kama ugaidi wa ndani.

Amesema kuwa ni siku ya huzuni kwa Marekani. Watumishi hawa wameihudumia nchi kwa heshima kubwa na kwamba tukio hili ni la ugaidi wa ndani.