CECAFA:Yanga kumenyana na Gor Mahia

Image caption Mashabiki

Huku michuano ya kombe la CECAFA mwaka huu ikianza siku ya jumamosi mjini Dar es Salaam,mechi tatu zitachezwa lakini kati yazo hakuna iliojaa mbwembwe kama ile ya Yanga ya Tanzania dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Timu hizo mbili zinakutana katika uwanja wa kitaifa wa Dar es Salaam zikipanga kuanza vyema mashindano hayo.

Image caption Yanga vs Simba

Yanga FC inarudi katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 wakati ambapo timu hiyo ilishinda michuano hiyo ilipoandaliwa Tanzania,lakini dhidi ya Gor Mahia wanakabiliwa na kibarua kigumu.

Gor Mahia inatarajiwa kushangiliwa na wafuasi wa mahasimu wa Yanga, Simba na tayari wameapa kuvaa jezi nyeupe wakati wa kipute hicho.