Duka la Westgate kufunguliwa leo

Haki miliki ya picha
Image caption Duka la Westgate kufunguliwa leo

Duka la westagate lililo mji mkuu wa Kenya Nairobi linafungua milango yake hii leo kwa umma karibu miaka miwili tangu lishambuliwe na wanamgambo wa al shabab.

Watu 67 waliuawa wakati wa makabiliano ya siku nne wakati wanamgambo hao walipowafyatulia risasi wateja.

Duka hilo linafunguliwa wiki moja baada ya rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara nchini kenya hatua inayoonekana kama ishara ya imani kwa usalama wa nchini Kenya.

Al Shabab wameendesha mashambulizi mengine mabaya nchini Kenya tangu litokee shambulizi la Westgate likiwemo la chuo kikuu cha Garissa ambapo watu 150 waliuawa.