Bi Sarah Obama
Huwezi kusikiliza tena

Kogelo yajiandaa kumkaribisha rais Obama

Ziara ya Rais Barack Obama nchini Kenya imevutia hisia mbalimbali miongoni mwa Wakenya. Ingawa amewahi kutembelea nchi hiyo ambako alizaliwa baba yake mara kadhaa miongo iliyopita akiwa mwanafunzi, wakili na Seneta; lakini yeye kufika kama Rais wa taifa lenye uwezo mkubwa zaidi duniani kumefanya wengi katika kijiji cha baba yake cha Kogelo, Magharibi mwa Kenya, kuendelea nas mipango ya kumkaribisha huko licha ya Ubalozi wa Marekani kudai kuwa ratiba yake haitamruhusu kufika huko. Muliro Telewa ametembelea alikozaliwa baba wa Rais Obama, Barrack Obama Senior, na kutuandalia ripoti ifuatayo.)