Pele alazwa hospitalini Sao Paulo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pele

Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya Brazil Pele amefanyiwa matibabu hospitalini miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume.

Vyombo vya habari vinasema kuwa Pele mwenye umri wa miaka 74 alikuwa akiugua mshipa wa damu uliokunjika na alifanyiwa upasuaji katika sehemu yake ya mgongo katika hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo.

Pele ambaye alishinda kombe la dunia mara tatu alitibiwa maambukizi katika sehemu ya kupitishia mkojo miezi minane iliopita baada ya figo yake kutolewa mawe.

Anatarajiwa kutoka hospitalini siku chache zijazo kulingana na ripoti.

Mirtes Bogea ambaye ni msemaji wa hospitali hiyo amesema kuwa amekatazwa kusema ni lini Pele alilazwa na kwa nini.