Casilla achukua nafasi ya Casillas R Madrid

Image caption Kiko Casilla

Real Madrid imemsajili kipa wa Espanyol Kiko Casilla kwa pauni milioni 4.2.

Real ilisalia na haki za asilimia 50 za umiliki wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 wakati alipoondoka kujiunga na Espanyol mwaka 2007.

Casilla ambaye ameandikisha sahihi ya miaka 5,atatoa ushindani mkubwa kwa kipa Keylor Navas na Fernando Pecheco.

Real ambayo ilimuuza kipa wa mda mrefu Iker Casillas katika kilabu ya Porto mwezi huu,pia wanamwinda kipa wa Manchester United David De Gea.