Saudia yawakamata wanachama 430 wa IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mfalme wa Saudia

Mamlaka nchini Saudi Arabia inasema kuwa imewakamata zaidi ya washukiwa 430 wa kundi la Islamic State wakati wa msako wake.

Wizara ya maswala ya ndani nchini humo inasema kuwa wanachama wa kundi hilo walikuwa wanapanga kuzua ghasia na kwamba njama kadhaa tayari zimetibuliwa.

Mipango hiyo ni pamoja na ule unaolenga ubalozi mmoja,mauaji ya maafisa wa usalama mbali na kutekeleza milipuko ya kujitolea muhanga ndani ya misikiti.

Kundi hilo limekiri kutekeleza mashambulizi ya mabomu mongoni mwa misikiti ilio na waislamu wa madhehebu ya shia mashariki mwa taifa hilo mnamo mwezi Mei.

Watu 25 waliuawa.