Nigeria yawika katika tuzo za MTV 2015

Image caption Baadhi ya wasanii walioshiriki katika tuzo za mama mtv nchini Afrika kusini

Wanamuziki kutoka Nigeria kwa mara nyengine tena wamewika katika sherehe za tuzo za MTV Awards mwaka 2015 zilizoandaliwa katika eneo la KwaZulu-Natal ikinchini Afrika kusini.

Tuzo hizo ziliwaleta pamoja wasanii wa ubunifu na muziki kutoka barani Afrika huku wengine wakifanya maonyesho ya muziki uliowavutia wengi.

Wale walioshinda usiku huo ni wasanii wa Nigeria akiwemo Yemi Alade na Davido ambao walijishindia tuzo za mwanamuziki bora wa kike na wakiume mtawalia huku nyota wa hip hop Cassper Nyovest akijishindia taji la mwanamuziki bora wa mtindo wa hip hop.

Image caption Msanii D Banj kutoka nchini Nigeria

D'Banj naye alishinda tuzo la mageuzi,likiwa ni tuzo jipya ambalo hupewa wanamuziki wa siku nyingi ambao wamewika katika utamaduni wa muziki wa Afrika.

Wawakilishi wa eneo la Afrika mashariki akiwemo msanii Diamond kutoka nchini Tanzania alishinda tuzo la Best Live music huku Sauti Sol Wakenya wakishindwa kupata tuzo lolote.

Nicki Minaj alishinda tuzo la mwanamuziki bora wa kimataifa huku kundi la P square likishinda tuzo la kundi bora zaidi la muziki na wasanii wa muongo huu.

Sherehe hiyo ilikuwa na maonyesho ya wasanii kama vile P Square walioimba nyimbo kama vile Chop my Money,Alingo na Shekini.

Tuzo hizo zilifanyika sawa na siku ambayo raia wa Afrika kusini husherehekea siku ya kuzawaliwa kwa marehemu Nelson mandela swala lililogusa myoyo ya wasanii wengi.

Hivi ndivyo wanamuziki hao walivyotuzwa .

Best Female: Yemi Alade (Nigeria)

Best Male: Davido (Nigeria)

Best Group: P-Square (Nigeria)

Best New Act Transformed by Absolut: Patoranking (Nigeria)

Best Hip Hop: Cassper Nyovest (South Africa)

Best Collaboration: AKA, Burna Boy, Da LES & JR: "All Eyes On Me" (SA/Nigeria)

Song of the Year: Mavins: "Dorobucci" (Nigeria)

Best Live: Diamond Platnumz (Tanzania)

Video of the Year: "Nafukwa" - Riky Rick; Director: Adriaan Louw

Best Pop & Alternative: Jeremy Loops (South Africa)

Best Francophone: DJ Arafat (Ivory Coast)

Best Lusophone: Ary (Angola)

Personality of the Year: Trevor Noah (South Africa)

MAMA Evolution: D'Banj (Nigeria)

Best International: Nicki Minaj

Artist of the Decade: P-Square