TRUMP:McCain sio shujaa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Donald Trump

Mfanyibiashara bilionea wa Marekani Donald Trump amezua tetesi kwa mara nyingine tena, baada ya kutilia shaka rekodi za vita za mmoja wa wamgombea wa zamani wa Urais wa chama cha Republican John Mc Cain.

Aliambia waumini waliokusanyika kwa kikao cha kidini kuwa Mc Cain ni shujaa wa vita, kwa sababu aliwahi kukamatwa nchini Vietnam lakini akaongeza kuwa yeye anapendelea zaidi wale wanajeshi ambao hawakukamatwa.

Haki miliki ya picha US GOV
Image caption John McCain

Pia alimkosoa kwa kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2008.

Awali seneta Mc Cain alimshutumu bwana Trump kwa kuchochea chuki miongoni mwa jamii ya wahamiaji nchini Marekani kutokana na matamshi yake dhidi yao.

John McCain alishikiliwa mateka kwa miaka mitano nchini Vietnam baada ya ndege yake ya kivita kuangushwa wakati wa vita.