Carter kuizuru Israel hii leo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Carter kuizuru Israel hii leo

Waziri wa Ulinzi wa Marekani amepangiwa kuzuru Israel hii leo, ikiwa ni kuanza kwa ziara yake ya mashariki ya Kati. Baadaye pia anatarajiwa kuzuru Jordan an Saudi Arabia.

Ziara hii inatazamiwa kuwa juhudi za kubembeleza, kwa nchi ambazo zimeelezea wasiwasi kutokana na mkataba wa Nuclear uliosainiwa juu ya Iran.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri huyo , Ashton Carter atakutana kwanza na maafisa wa Israel kabla ya kukutana rasmi na waziri mkuu Benjamin Netanyahu siku ya Jumanne.

Bwana Netanyahu amekashifu mkataba huo wa Iran kuwa makosa makubwa ya kihistoria, akisema kuwa yataipatia Iran Kiburi cha kiuchumi na kisiasa.