Jaji aruhusu kesi ya 50 cent kundelea

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jaji aruhusu kesi dhidi ya 50 cent kundelea

Jaji mmoja nchini Marekani ameamua kwamba kesi kuhusu mkanda wa video ya ngono inaweza kuendelea dhidi ya mwanamuziki wa mitindo ya kufoka 50 Cent.

Kesi hiyo itaendelea mbele na kusikizwa licha ya mwanamuziki huyo kuwasilisha mahakamani madai ya kufilisika.

Jopo la wazee wa mahakama ya New York lilimzawadia Lastonia Leviston $5m (£3.2m) wiki iliyopita.

Jopo hilo liliamua kuwa msanii huyo wa muziki ya kufoka , ambaye jina lake sahihi ni Curtis Jackson III, hakua na ruhusa kutoka kwa Lastonia Leviston alipoweka picha za video za ngono zilizochukuliwa alipokua na mpenzi wake wa kiume.

Jopo hilo la mahakama linatarajiwa kuangalia suala la hasara iliyosababishwa na hatua hiyo kwa pande zote mbili Jumatatu .

Wakili wa Lastonia Leviston alidai kuwa 50 Cent aliwasilisha mahakamani madai ya kufilisika kuepuka kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Wiki iliyopita wakopeshaji wa mwanamuziki huyo walifichua taarifa kuhusu madeni yake baada ya kuwasilisha madai yake ya kufilisika.

Miongoni mwa madeni yake ni ada ya umeme ya kasri lake ya dola elfu tano $5,649 na takriban dola laki moja elfu thelathini na saba na mia nane themanini, $137,880.