Burundi:AU huenda isishiriki uchaguzi

Image caption AU huenda isishiriki uchaguzi wa urais wa Burundi hapo kesho

Yaelekea Muungano wa Afrika hautaweza kupeleka wanajeshi na waangalizi wa haki za kibinadamu nchini Burundi kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika kesho Jumanne.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari, Muungano huo wa Afrika wanasema kupelekwa kwa maafisa hao kumesababishwa na masharti mapya ya Burundi kwamba waangalizi sharti wawe na vibali vya kuingia Burundi mbali na vyeti vyao vya kusafiria vya kibalozi.

Image caption Mazungumzo baina ya serikali na upinzani yalivunjika mwishoni mwa juma

Mazungumzo baina ya serikali na upinzani yalivunjika mwishoni mwa juma baada ya pande hizo mbili mbili kushindwa kufikia makubaliano.

Upinzani unadai kuwa rais Nkurunziza anakiuka katiba ya taifa na mapatano ya Arusha yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Image caption Burundi imeweka masharti mapya dhidi ya maafisa wa AU

Burundi imezama katika mgogoro wa kisiasa uliokumbwa na ghasia tangu rais wa nchi hiyo kutangaza kugombea nia ya kuwania muhula wa tatu .

Zaidi ya raia laki moja wa Burundi wamekimbia nchi hiyo tangu mwezi Aprili kulipozuka ghasia kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.