FIFA kupanga tarehe ya uchaguzi wa rais

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa FIFA Sepp Blatter

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter na bodi ya utawala ya shirikisho hilo pamoja na viongozi wengine wa juu wa shirikisho hilo wanakutana leo kupanga tarehe ya uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo.

Blatter alitangaza mwezi uliopita kuwa atajiuzulu kama rais wa FIFA baada ya wiki ya tuhuma za ufisadi kwa baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo.

Baadhi walitiwa mbaroni na maafisa usalama kutoka Marekani kwa ajili ya uchunguzi wa rushwa.

Mkutano huo wa leo pia unatarajia kutaja baadhi ya mambo yatakayorekebishwa ikiwa ni pamoja na kikomo cha urais na viongozi wengine wa juu wa shirikisho hilo, pamoja na kuchapisha mishahara na marupurupu ya viongozi wa juu wa shirikisho hilo.