Man U yasema haitaongeza mshambuliaji

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kocha Mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal

Kocha mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal ametamba kuwa hatanunua mshambuliaji mwingine kwani alio nao kwa sasa wanatosha wakiongozwa na Wayne Rooney.

Pamoja na Wayne Rooney washambuliaji wengine waliobaki ni Javier Hernandes Chicharito, na James Wilson baada ya mshambuliaji mpachika magoli Robin Van Persie kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki hivi karibuni na Radamel Falcao mkopo wake kumalizika.

Van Gaal anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji pekee pale mbele ambapo atasaidiwa na Mephis Depay aliyesajiliwa wakati wa majira ya joto kutoka PSV Eindhovenya Uholanzi.

Van Gaal anatamba kuwa Depay anaweza kuwa mshambuliaji wa katikati tofauti na alivyokuwa akitumika wakati alipokuwa PSV.