Brazil inachunguza mauaji ya watu 35

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi nchini Brazil

Mamlaka nchini Brazil katika mji wa Manaus wameanzisha uchunguzi kufuatia mauaji mabaya ambapo zaidi ya watu 35 wameripotiwa kuuwauwa kati ya ijumaa na jana Jumatatu asubuhi.

Mauwaji hayo yalianza baada ya sajenti mmoja wa polisi kupigwa risasi nje ya Benki.

Manaus ilikuwa miongoni mwa miji ambapo kombe la dunia mwaka 2014 ilichezwa na itakuwa mwenyeji wa michuano ya Olympic mwaka 2016.

Mauaji hayo yalianza siku ya ijumaa usiku katika mji huo wa Manaus alipo katika kitovu cha Amazon. Siku ya jumatatu watu thelathini na watano waliuawa. Vikosi vya usalama wa raia vinafuatilia ambapo vinaendesha uchugunzi kuhsusu chanzo cha mauaji hayo.

Idara ya Polisi inaamini kuwa mauwaji hayo huenda yamesababishwa na maafisa waliokuwa wakilipiza kisasi au kutekelezwa na magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Mauaji hayo yametokea kwa wakati mmoja kwa waliuawa kupigwa risasi katika maeneo mbali mbali ya mji huo ikiaminika vikundi tofouti vinahusika na vitendo hivyo.