Ndege ya Lufthansa yaponea ajali

Ndege ya kampuni ya Lufthansa
Image caption Ndege ya Kampuni ya ndege ya ndege ya Ujerumani -Lufthansa iliyoponea ajali

Ndege ya kampuni ya Ujerumani Lufthansa nusura igongane na ndege isiyo na rubani ilipokuwa ikikaribia kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Warsaw nchini Poland, kwa mujibu wa maafisa.

Tukio hilo lilitokea Monday mchana wakati ndege isiyokuwa na rubani ilipokuwa kuja mita 100 kutoka kwenye ndege ya Lufthansa iliyokuwa ikitokea Munich, Ujerumani , ameeleza msemaji wa uwanja huo.

Muhudumu wa ndege ya Lufthansa Embraer chapa ERJ-195 aliripoti tukio hilo

Msemaji wa uwanja wa ndege mjini Munich anasema polisi wanachunguza tukio hilo.

Haki miliki ya picha Lufthansa
Image caption Uchunguzi unafanyika kubaini kwanini ndege isiyokua na rubani ilipita njia ya ndege ya Lufthansa

Mikolaj Karpinski, wa shirika la huduma za safari za anga la Polando , ameiambia televisheni ya Poland kuwa rubani ali ripoti mara moja kwa waangalizi wa safari za ndege zisizokua na rubani , ambao waligeuza njia ya ndege.

Ndege Lufthansa iliendelea na safari yake na kutua salama takriban dakika tatu baadae.