Askofu Desmond Tutu apata afueni

Askofu mkuu mstaafu wa Afrika kusini Desmond Tutu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Askofu mstaafu wa Afrika kusini Desmond Tutu ameondoka hospitalini baada ya matibabu ya saratani

Askofu mkuu mstaafu wa Afrika kusini Desmond Tutu, kwa jina maarufu ''Arch'' ama safina, sasa amerejea nyumbani baada ya kuwa hospitalini kwa wiki nzima ambako alikua akitibiwa kwa maambukizi makali , kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakfu wa Tutu.

Mwanae wa kike , Mpho Tutu, amesema kuwa madaktari wamemshauri apumzike sana: '' Tunaendelea vizuri na tutafanya kila tuwezalo tusiwaangushe".

Image caption Madaktari wamshauri Askofu mstaafu wa Afrika kusini Desmond Tutu apumzike sana

Kauli ya Wakfu wa Tutu imesema kuwa amerudi nyumbani akiwa amevalia gauni lenye maneno '' Pona haraka Safina'' " nyuma yake, ikitoa ujumbe kwamba mzee huyo mwenye umri wa miaka 83 anahitaji kupumzika.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Askofu Desmond Tutu amekuwa akilazwa mara kwa mara

Askofu Desmond Tutu, amekuwa akilazwa hospitalini mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni na amekua akitibiwa maradhi ya saratani ya tezi dume.