Buhari tayari kuzungumza na Boko Haram

Mahammadu Buhari Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Nigeria Mahammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram ili wawaachilia wasichana wa wa shule 219 waliotekwa nyara kutoka kwenye shule yao ya malazi mnamo mwaka 2014.

"Kama tunaamini kuwa uongozi wa Boko Haram unaweza kuwaachilia huru na salama wasichana hao tunaweza kujiandaa kufanya kuzungumzia nini wanachokitaka ," alikua akizungumza katika mahojiano na televisheni ya Marekani CNN.

Haki miliki ya picha .
Image caption Rais wa Nigeria Mahammadu Buhari akiwa na rais Obama wakati wa ziara yake nchini Marekani

Kundi la wanamgambo wa kiislam la Boko Haram limekua likiendesha mashambulizi ya mara kwa mara katika maeneo ya kaskazini mwa Nigeria na serikali imekuwa ikilaumiwa kwa kutoweza kuwadhibiti wanamgambo hao wa kiislam wenye itikadi kali.