Human Right Watch yaituhumu Sudan Kusini

Image caption Sudan kusini

Shirika la Human Rights Watch limevituhumu vikosi vya jeshi la Sudan kusini, kwa mauaji, ubakaji na uchomaji wa mali za raia.

Shirika hilo la la Haki za Binadamu limelaumu pia vikundi vya wanamgambo vinavyoungwa mkono na serikali ya Sudan kusini kwa matukio hayo.

Shirika hilo limesema wakosaji hao wamekiri uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mashuhuda wa matukio hayo wamewaambia watafiti wa ripoti hiyo kwamba raia wamekuwa wakishambuliwa na vifaru na kuchomwa moto wakiwa hai.

Uovu huo umetokea wakati majeshi yanayomtii Rais Salva Kiir kushambulia sehemu kubwa ya jimbo analotoka kiongozi wa waasi Riek Machar.

Serikali ya Sudan Kusini imekana ripoti hiyo ya udhalilishaji na dhuluma inayodaiwa kufanywa na jeshi lake.