Ugiriki yakubali masharti ya wadeni

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras

Wabunge wa Ugriki wamepiga kura kuunga mkono masharti mapya yaliyowekwa na wadeni wa taifa hilo lililo katika hatari ya kufilisika.

Hatua hiyo inatoa nafasi kuanzishwa kwa mashauriano mapya kati ya taifa hilo na mataifa yanayotoa msaada wa kuokoa uchumi kuanza.

Waziri Mkuu, Alexis Tsipras, alishinda kura hiyo ya Bunge baada ya kura ya kuunga mkono kupigwa na vyama vingine vya upinzani..