Ukulima wa Mawese Liberia wazuliwa baa

Haki miliki ya picha rajanaidu
Image caption zao la Mawese nchini Liberia

Shirika moja la kujtetea haki limeihsutumu mojawepo ya kampuni kubwa zaidi duniani ya mauzo ya mawese, iliyoko nchini Liberia, kwa kutumia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kujitajirisha.

Shirika hilo, Global Witness, limesema kuwa wakati mlipuko huo ulipokuwa kilele Afrika Magharibi mwaka uliopita, kampuni ya Golden Veroleum ilifyeka maelfu ya ekari kwa maandalizi ya upanzi wa mmea huo wakati ambapo makundi ya missada kwa jamii yalikuwa yanashughulika na kuokoa maisha ya watu kutokana na ugonjwa huo.

Hata hivyo kampuni hiyo imejibu katika barua walioandika kwa shirika hilo la Global Witness kuwa kandarasi ya pekee waliosaini mwaka huo, ilitokana na kazi zao za miezi au hata miaka kabla ya kuzuka ugonjwa huo.

Haki miliki ya picha rajanaidu
Image caption shamba kubwa la Mawese Liberia

Wanaharakati wa mazingira wamekuwa wakilaumu wakulima wa mashamba makubwa ya mawese kwa uharibifu wa mazinginra na ongezeko la joto duniani.