''Museveni'' atoa wimbo mpya wa kampeni

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wimbo mpya wenye sauti ya rais Museveni unasikilizwa na waganda

Wimbo mpya umetolewa nchini Uganda mwimbaji akiwa rais wa Uganda Yoweri Museveni .

Lakini bado bado haijafahamika wazi ikiwa yeye binafsi ndie aliyeutoa ama alishiriki katika kuutoa.

Hata hivyo kuna tetesi kwamba ni wimbo mpya wa kampeni za uchaguzi mkuu ujao 2016.

Sauti bila shaka ni rais Museveni, wimbo unaitwa Yegoma. Maana yake kwa taji --- kama la ufalme.

Maneno ya wimbo yanelezea uchungaji wa ngombe , ala za muziki na maisha marefu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wengi wanahisi wimbo mpya wa unahusiana na kampeni za uchaguzi mkuu wa 2016

Beti ya kwanza inasema (Oruyogo-yongo - orwa Kabale) ikimaanisha usisalimu amri.

Katika picha ya Video ya wimbo huo inaonyesha ndege aina ya Kulastara akijaribu kummeza chura, lakini chura anamkaba ndege kooni.

Oruyongoyongo ni ndege anayekula nyoka na panya.

Image caption Wimbo ''Yegoma'' umetolewa wakati rais Museveni akikabiliwa na upinzani ndani ya chama chake cha NRM

Na katika ubeti wa mwisho Rais anazungumzia maisha marefu na kuwaambia wasikilizaji kwamba wimbo kama Yengoma na Mpenkoni zinatakiwa kubaki katika jamii wakimukumbuka.

Wimbo wa ''Mpenkoni'' yaani nipe fimbo, ulitumiwa na katika kampeni bwana Museveni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2011.

Wimbo huu mpya umetolewa ikiwa rais Yoweri Museveni anakabiliwa na upinzania mkubwa katika chama chake tawala cha NRM.

Aliyekuwa waziri wake mkuu Amama Mbabazi na makamu wake wa zamani Prof.Gilbert Bukenya wametangaza nia ya kugombea kiti cha urais kwa chama tawala anachokiongoza rais Museveni.