Je ziara ya rais Obama itaifaidi nini Afrika

Image caption Barack Hussein Obama ni rais wa kwanza, aliyeko madarakani, kuizuru Kenya.

Barack Hussein Obama ni rais wa kwanza, aliyeko madarakani, kuizuru Kenya.

Rais Obama ameitembelea Afrika mara kadha awali, kwa kwenda Misri, Ghana, mwaka 2009, mwaka 2013 alizuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.

Wadadisi wanadhani ziara yake ya Kenya huenda ikawa ya mwisho katika bara la Afrika kama rais.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption “Hakuna mtu yeyote Mwafrika kama Barack Obama”

Lakini atawaachia nini iliwaweze kuimba “Hakuna mtu yeyote Mwafrika kama Barack Obama”?

Mwandishi wetu wa maswala ya kiuchumi , Alli Mutasa, aeleza kutoka mjini Kampala Uganda.

Wakenya hawana muhali, kwani hata jina Barack Obama ni raslimali kwao, kwa mujibu wa maneno ya waziri wa nchi za nje wa Kenya, Amina Mohamed.

''Amekuwa, ndiye bidhaa bora zaidi Kenya kuwahi kuwa nayo.'' anasema Waziri Amina Mohamed.

Image caption Lakini atawaachia nini iliwaweze kuimba “Hakuna mtu yeyote Mwafrika kama Barack Obama”?

Ikiwa WaIrish walidiriki kumuimba ‘hakuna mtu M-Irish kama Barack Obama’ alipozuru kisiwa cha Ireland, iweje sisi Wafrika tushindwe kumuimba.

Na tumemuimba - Kaskazini na Kusini, Magharibi na hususan Mashariki mwa Afrika.

Samba Mpangalala'' Obama anahudumia muhula wake wa pili na mwisho, na sisi tunaachana na kisasili na sasa tunawazia kwa dhati, urathi wa Obama, kwa Afrika.

Kwa kauli yake mwenye, alipozuru Afrika mwaka 2013, alieleza kiini cha mtazamo wake kuihusu Afrika''

'' Kanuni ilioongoza mtazamo wangu kwa Afrika tangu niwe Rais, kwamba usalama na ustawi na haki tunavyosaka duniani, haviwezi kupatikana bila ya Afrika imara na iliostawi na yenye kujitegema.

Image caption Kwa mengi aliokuwa nayo nyumbani, Afrika ilishika nafasi ya nyuma muhula wa kwanza.

''Ni kwa njia hii tunaweza kuelewa urathi wake,kama upo, kwa Afrika.

''Aliingia madarakani wakati Afrika ikiwa huru, vita baridi vikiwa vimekwisha, na sasa dunia nikijiji''

Kwa mengi aliokuwa nayo nyumbani, Afrika ilishika nafasi ya nyuma muhula wa kwanza.

Angalau Afrika ilikuwa na Rrais Marekani, ambaye asingepinga kitu chema kwa maendeleo ya Afrika.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Marekani inafaidika zaidi katika urari wa biashara,lakini kiwango cha biashara ni chini ikilinganishwa na biashara kati ya Uchina na Afrika

Kuna msururu wa juhudi zilizozinduliwa katika ikulu ya White House, hasa katika muhula huu wa pili, ikiwemo miradi ya kilimo, nishati na biashara.

Aidha mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika – mbali ya USAID, Agoa, na misaada ya dharura ya kupambana na ukimwi.

Biashara baina ya Afrika na Marekani imeongezeka; mwaka wa 2014, ilifikia dola bilioni $73 – kati ya hizo, zaidi ya dola bilioni $38 ni mahuruji ya Marekani na karibu $35bn, maduhuli kutoka Afrika.

Ni Marekani inayofaidika zaidi katika urari wa biashara, lakini ni kama ndo-ndo-ndo ikilinganishwa na kiwango cha biashara baina ya Uchina na Afrika, ambayo 2014 ilikuwa dola bilioni $222bn.

Image caption Marekani inaendesha kambi ya kijeshi nchini Djbouti

Hata katika sekta ya usalama ambako Marekani inaongoza katika zana na wanajeshi, Uchina imeanza kujiingiza katika sekta ya usalama, ikiwa na wanajeshi Sudan Kusini na pia itajenga kituo cha wanamaji nchini DJibouti, huku pakiwa tetesi za uwezekano Uchina kuwa na kituo kingine kituo katika Zimbabwe.

Katika nyanja hizo mbili, kijeshi na kiuchumi, uingiliaji wa Marekani na Uchina, mataifa mawili makuu kiuchumi duniani, utazidi katika Afrika.

Na ziara ya Obama nchini Kenya si tu ya kinasaba, bali ni chombo cha kuzika milele hisia za Wafrika kuwa Marekani ni kipingamizi kwa ‘Afrika yainuka’ kiuchumi.

Na kama wawekezaji wa Marekani kwa wingi watafuata kisogo chake Kenya na nchi nyengine za Afrika, huo utakuwa urathi wa kipekee.