2 wauawa katika shambulio jipya Marekani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bendera ya Marekani

Polisi katika jimbo la Louisiana nchini Marekani wamesema kuwa mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki amewafyatulia risasi raia katika ukumbi wa sinema na kumuua mtui mmoja. Watu wengine ssita wamejeruhiwa , na mshambuliaji mwenyewe pia amejiua.

Walioshuhudia wanasema kuwa walimuona mtu mmoja, mzungu wa umri wa miaka 50 au zaidi, amejitokeza kunako dakika ishirini baada ya filamu kuanza , filamu ya Train wrek, na kisha kuanza kufyatua risasi kiholela. Mmoja anasema kuwa alisikia mlipuko kama vile baruti.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi wazingira eneo la ufyatiliaji wa risasi Marekani

Polisi wamezingira eneo la tukio huku Gavana wa jimbo hilo akisema kuwa anaelekea huko kujikagulia mwenyewe hali iko vipi.

Hili imetokea saa chache tu baada ya Rais Barack Obama kuzungumzia tatizo la udhibiti wa silaha nchini Marekani. Katika mahojiano maaluma na BBC , Rais Obama amesema kushindwa kudhibiti silaha nchini mwake ni jambo lililomsononesha katika utawala wake.

Image caption Bunduki za Marekani zinahitaji udhibiti

Amesema Marekani ni nchi pekee iliyoendelea ambayo haina sheria ya kutosha kuhusu usalama wa silaha, hata wakati huu ambapo kumekuwa na marudio ya matukio ya mauaji.

Obama amesema magaidi wamewaua chini ya wamarekani 100 tangu shambulio la kigaidi la Septemba 11, lakini waliouawa kwa matukio ya kutumia silaha ni makumi kwa maelfu katika kipindi hicho.

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Obama akihutubia bunge la Congress juu ya silaha

Rais Obama alijaribu kusukuma mbele sheria ya udhibiti wa silaha baada ya tukio la mauaji kwenye shule moja inayojulikana kwa jina la Sandy Hook School mwaka 2012, lakini sheria hiyo ya kubana matumizi ya silaha ilikataliwa na bunge la Congress.