Je Afrika imefaidika na mpango wa AGOA ?

Image caption Je Afrika imefaidika na mpango wa AGOA

Ushawishi wa Marekani kwa umeenea kote duniani.

Ukitazama utamaduni wa Marekani, umesafiri kote, na katika bara Afrika, bidhaa kutoka Marekani nazo zinapatikana karibu kwa kila kijiji.

Lakini kuna maeneo mengine, angalau bidhaa za Marekani hazijatawala.

Kufuatia ziara ya rais wa Marekani Barack Obama nchini Kenya na Ethiopia kuanzia leo , mwandishi wetu wa Afrika, Andrew Harding, amekua akikagua ushawishi wa Amerika katika bara Afrika, kutoka Lesotho, na hii hapa tathmini yake ikisomwa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Je uwekezaji wa China umeathiri ushawishi wa Marekani barani Afrika ?

Katika kijiji kidogo nchini Lesotho, katika duka moja kubwa la bidhaa linalomilikiwa na raia wa China, kwenye ukuta kuna televisheni inayopeperusha kipindi kutoka China.

Vilevile kuna mikate inayotengenezwa na kiwanda kimoja hapa lesotho kinachomilikiwa na mchina, ni wazi kwamba Uchina inatawala kwa kiwango kikubwa barani Afrika

"jamaa zangu wamekuwa hapa kwa miaka kadhaa, na waliniambia kuwa mazingira ni mazuri na kwa hivyo niliamua kuhamia huku" anasema mfanyibiashara huyo kutoka Uchina

''Hapa watu wanatuheshimu kwa kiwango fulani, kwa sababu sisi huwasaidia na wanahisi sisi tuko sawa kama watu''

Image caption Je uwekezaji wa China umeathiri ushawishi wa Marekani barani Afrika ?

Nipo katika mji mkuu Maseru, Lesotho, kuna mwanafunzi ambaye amezuru kliniki hii inayoshugulikia waathiriwa wa Ukimwi kwa ushauri.

Takriban robo ya idadi ya watu nchini humu, wameathirika na janga hili la Ukmwi na mumiliki wa kliniki hii, si mchina, anatoka Marekani anayejulikana kama daktari Edith Mohapi, daktari wa watoto.

''Tukiangazia vita dhidi ya Ukimwi, kuna umuhimu wa usaidizi kutoka nje,''

''watu wengi wangekuwa wamekufa, kwa sababu watu wengi hawawezi kumudu dawa za kupunguza makali ya Ukimwi,

Image caption Maelfu ya wa waafrika wameajiriwa kutokana na AGOA

''Kwa hivyo Marekani imewasaidia sana.'' anasema daktari Mohapi.

''kila ambaye anaugua Ukimwi anatibiwa bila malipo'' anaongezea.

Katika kiwanda cha kushona nguo,za majira ya baridi, mamia ya wanawake wanashona nguo za kusafirisha ng'ambo.

Hapa ndipo Marekani na China zinapatana, hapa kampuni nyingi za Uchina zinafaidika kutokana na mpango wa kibiashara unaowezesha mataifa ya Afrika kusafirisha bidhaa Marekani bila ushuru maarufu kama AGOA

Mpango ambao umewezesha maelfu ya watu kupata ajira.

kutana naye Motebang Mokoaleli, ambaye ni mkuu wa mipango na utafiti katika kampuni moja ya kuhamasisha uwekezaji hapa Lesotho.

Image caption Mpango ambao umewezesha maelfu ya watu kupata ajira.

Anasema kuwa wawekezaji wengi nchini Lesotho, wanaoingiza bidhaa zao katika soko la Marekani, ni wa asili ya Asia.

Maoni yake ni kuwa wawekezaji wengi kutoka Marekani hawana habari kuwa maeneo kama haya yapo duniani, na tuna jukumu kubwa sana la kujulisha Marekani kwamba maeneo kama haya yapo, na tuna uwezo.

Bila shaka sasa China ipo kila mahali barani Afrika ?

Image caption Bila shaka sasa China ipo kila mahali barani Afrika

''Wako kila mali, nadhani wamekuwa magwiji katika biashara''

Ili kusisitiza uwepo Wachina, makao ya mayatima kusini mwa mji mkuu wa Lesotho, Maseru, kunafunzwa mojawapo ya lahaja ya lugha ya Kichina maarufu kama Mandarin.

Mradi huo unomilikiwa na raia wa Taiwan

Umuhumi wa Marekani hapa Lesotho na kote barani Afrika, unabakia kuwa wa maana sana, lakini mashinani, inchi za Asia zinazidi kunawiri katika pembe zote za Afrika