Obama leo kuhutubia wajasiriamali Kenya

Haki miliki ya picha AFP GETTY
Image caption Rais Barack Obama alipowasili Kenya hapo jana

Rais wa marekani Barack anatarajiwa kuhutubia kongamano la wajasiriamali akianza rasmi ziara yake katika eneo la afrika masharaki.

Anatarajiwa kuzungumzia suala la ufisadi ambapo atataka kuwepo kwa jitihada kubwa za kupambana na ufisadi na pia kuwahutubia wafanyibiahara vijana nchini Kenya.

Obama baadaye atatembelea eneo kulikotokea shambulizi la kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa marekani mjini Nairobi na pia kukutana na rais wa kenya uhuru kenyatta kwa mazungumzo ambapo wataangazia usalama wa kanda hiyo na tisho kutoka kwa kundi la kigaidi la Al shabaab.

Marekani imekuwa ikiisadia kenya katika vita dhidi ya ugaidi na imewaua vongozi kadha wa kundi la al shabaab kwenye mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani.