ZIARA YA RAIS OBAMA NCHINI KENYA

RAIS BARACK OBAMA KUHUTUBIA WAKENYA KATIKA UWANJA WA KASARANI LEO JUMAPILI

08:10 JUMAPILI: Rais Barack Obama asubuhi anatarajiwa kuwahutubia Wakenya katika uwanja wa Kasarani nje kidogo ya jiji la Nairobi.

HABARI YA ASUBUHI-Jumapili tarehe 26

17.10pm:-Nchini Burundi nawataka viongozi kuketi chini na kujadiliana ili kupunguza umwagikaji wa damu wa aina yoyote.Kenya vilevile itashirikiana na Marekani katika kukabiliana na magonjwa ili kuzuia milipuko.Serikali haifai kuwatenga watu kulingana na jinsia zao kwa kuwa wao wana haki kama watu wengine.

Image caption Obama

17.01pm:-Tishio la Ugaidi-wakenya wameonyesha uvumilivu wa kukabiliana na tatizo hilo.Tunaishukuru Kenya kwa kuwahifadhi wakimbizi wengi wa Somalia.Tumezungumza kuhusu kukabiliana na itikadi kali.Mataifa yetu yatafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kufanikiwa

16.55pm:-Pia tunampango wa kushirikiana na serikali kuleta umeme katika maeneo ya mashamabani.kwa pamoja tunakabiliwa na tishio la maendeleo, nampongeza rais Uhuru kenyatta kukabiliana na Ufisadi.

16.53pm:-Ndege za moja kwa moja kutoka Marekani hadi Kenya-Tunataraji kwamba hili litaangaziwa na safari hizo kuanza hivi karibuni,lakini kuna baadhi ya maswala ambayo ni sharti yaangaziwe ikiwemo mambo ya usalama kabla hilo kutimizwa.Tutaongeza makubaliano yetu ya Agoa kwa miaka mingine kumi ili kuimarisha uhusiano wetu wa kibiashara.

16.50pm:Barrack Obama

Image caption Obama

Mazungumnzo yetu yanahusisha maslahi ya mataifa yetu.Mwanzo naipongeza Kenya kwa kuimarisha demokrasia nchini.Uchaguzi uliofanyika ulikuwa wa ushindani mkubwa na wa amani.Nitakutana na wawakilishi wa vyama vya kijamii kwa kuwa wao ni kitengo muhimu katika kupigania demokrasia.Vita dhidi ya wawindaji haramu-tuna mpango wa kuweka sheria inayopiga marufuku uuzaji wa pembe za ndovu.Hali ni mbaya nchini Sudan,tunataka viongozi wa taifa hilo kuweka taifa mbele.

16.47pm:-Marekani na Kenya zina utamaduni tofauti na kwamba kuna maswala muhimu yanayowaathiri wakenya kama vile afya ya uma njaa na umasikini,maswala ambayo yanapewa kipao mbele.Swala la wapenzi wa jinsia moja sio swala muhimu na haliwezi kupewa kipao mbele.

16.46pm:Uhuru-Hatuungi mkono wapenzi wa Jinsia moja

Image caption Uhuru Kenyatta

Tunazungumza kwa sauti moja kuhusu maswala mengi sana.Walio katika nyadhfa serikalini ni lazima wawajibike.Tumekubaliana kushirikiana katika mambo mengi ikiwemo kilimo,miundombinu na kawi kwa lengo la Kuimarisha mazingira yatakayovutia uwekezaji.

16.45pm:Obama na Uhuru wajitokeza kuhutubia vyombo vya habari

16.10pm:Mkutano na wanahabari

Image caption Ikulu

Mkutano na vyombo vya habari kufanyika mda wowote kuanzia sasa

15.25pm:-William Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC mjini the Hague.

15.30pm:Ruto na Obama

Image caption Ruto

Hatimaye naibu wa rais wa Kenya William Ruto amefanikiwa kusalimiana na rais wa Marekani Barrack Obama baada ya kukosekana hapo jana katika ujumbe uliomkaribisha rais huyo alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

15.15pm:Mkutano na wanahabari

Image caption Umati uliomsubiri Obama barabarani

Baada ya kikao hicho cha faragha kati ya serikali ya Kenya na Marekani Viongozi wa mataifa hayo Rais Barrack Obama na Mwenzake wa Kenya watafanya mkutano na wanahabari ili kuweza kutangaza yale walioafikiana katika mkutano huo wa kibiashara

15.00pm:Ikulu ya rais Nairobi kenya

Image caption Ikulu

Mkutano wa faragha wa kibiashara kati ya mataifa ya kenya na Marekani umeanza katika ikulu ya rais nchini Kenya.Rais Barrack Obama na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta wanawaongoza wajumbe kutoka mataifa hayo mawili katika mkutano huo.Swala la ugaidi ni miongoni mwa maswala tata yanayotarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho.

Image caption Watu waliovalia nguo zenye rangi za bendera ya Marekani

Rais ‪Obama‬ pia anatarajiwa kutia sahihi ya mikataba ya kibiashara na mwenyeji wake rais Kenyatta katika ikulu ya Nairobi

14.30pm:Ikulu ya rais Nairobi

Image caption Ruto

Rais Barrack Obama kukutana na naibu wa rais wa kenya William Ruto ambaye anakabiliwa na mashataka ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa ya ICC katika mazungumzo ya kibiashara kati ya Kenya na Marekani yatakayoandaliwa katika ikulu ya rais

13.50pm:Rais Obama akiweka maua

Image caption Obama

Rais Barrack Obama akiweka shada la maua katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa Marekani katikati ya jiji la Nairobi

13.25:Memorial Park

Image caption Obama
Image caption Obama

Rais Obama na Uhuru Kenyatta wawasili katika eneo la shambulizi la kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa Marekani katikati ya jiji la Nairobi.Baadhi ya barabara katika jiji la Nairobi zimebakia kuwa mahame

13.10pm:Manusura 1998

Image caption Manusura
Image caption manusura

Raia Walionusurika shambulizi la 1998 kenya wabeba mabango wakidai kwamba hawakufidiwa.Wanamtaka rais Obama kutowatupa na badala yake kuangalia maslahi yao.

12.45pm:Densi

Image caption Wachezaji densi
Image caption Nairobi

Wachezaji densi ya kimasai wakisubiri kumtumbuiza rais Barrack Obama aliyetarajiwa kuwatembelea katikati ya jiji la Nairobi

12.30pm:M-kopa

Image caption M-kopa

Rais Obama kwa sasa ametembelea maonyesho ya uvumbuzi jijini Nairobi ambapo alikutana na June Muli afisa anayesimamia maslahi ya wateja M-Kopa ambao hutoa huduma ya kawi ya jua ya 'pay as you go' katika makaazi.

11.10am:Memorial Park

Image caption Obama-uhuru

Obama na Uhuru sasa waelekea katika eneo la shambulizi la kigaidi la mwaka 1998 jijini Nairobi

10.55am:

Image caption Obama na Uhuru

Obama amaliza hotuba yake

10.50am:BBC hewani moja kwa moja

Image caption Obama

Runinga ya BBC inapeperusha moja kwa moja kongamano hilo hewani

10.48am:Mpesa

Image caption Obama

Kenya inaongoza katika teknolojia za kibiashara.Kwa mfano utumizi wa Mpesa-ni vyema kwamba teknolojia hiyo ilianza hapa Kenya

Image caption Obama akiwasikiza wajasiria mali

Obama 'Tutazindua mfuko wa kudhamini biashara zinazoanzishwa na wanawake

Kina mama ndio injini ya maendeleo barani Afrika.

Image caption Vibonzo nchini Kenya

Vituo vitatu vitafunguliwa Mali,Kenya na Zambia barani Afrika ili kuwasaidia wanawake wajasiriamali

10.41am:Rais Obama

Image caption Rais Obama

Rais Obama awasalimia wakenya kwa neno 'niaje' na

Hawayuni na kusema kuwa familia yake inatoka nchini kenya.

Lengo la mkutano huu aliouzindua miaka mitano iliopita mjini Washington ni kuwapiga jeki wafanyibiashara duniani.

Amesema kuwa kuna umuhimu wa kukabiliana na ufisadi ili biashara kushamiri.

10.35am:Uhuru Kenyatta

Image caption Obama

Kenya ilikumbwa na chanagamoto chungu nzima ikiwemo majanga lakini imesimama imara na kusonga mbele.

Bara la Afrika haliwezi kutegemea mataifa ya magharibi .

Taifa la kenya ni chimbuko la makabila tofauti.

Image caption Rais Obama

10.15am:Mkutano waanza

Mkutano wa wajasiriamali umeanza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia mkutano

10.00am:Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta

Image caption Uhuru Kenyatta

Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta ukiwa tayari umewasili katika eneo la mkutano wa wajisiriamali unaotarajiwa kufunguliwa na raia wa marekani Barrack Obama

09.45am:Waandishi

Image caption Waandishi habari
Image caption Waandishi

Waandishi wa habari wakijiandaa kuliangazia kongamano la kibiashara la wajasiriamali katika eneo la Gigiri jini Nairobi.Vifaa vya waandishi hao vimepekuliwa na maafisa wa usalama wa Marekani.

09.00am:Ndege Nairobi

Image caption Ndege za kijeshi

Ndege za kijeshi za Marekani zimeanza kuzunguka katika anga ya jiji la Nairobi kuimarisha usalama.

08.30am:Barabara za Jijini Nairobi:

Image caption barabara

Barabara nyingi za mji wa Nairobi zimeonekana kuwa bila watu na magari kufuatia kuwasili kwa rais Obama.Mapema leo maafisa wa polisi walionekana katika barabara zinazoelekea katika eneo la Gigiri ambapo rais Obama atafungua rasmi kongamano la kibiashara.

08.20am:Obama na familia yake

Image caption Sara Obama,Barrack Obama na Daktari Auma

Mama Sarah Obama,Rais Obama na dadaake Daktari Auma Obama wakijumuika katika chakula cha jioni katika hoteli moja jijini Nairobi.