Wakurdi wadai kushambuliwa na Uturuki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa kikurdi nchini Iraq

Kikosi cha wapiganaji wa Kikurdi kaskazini mwa Syria kimeishtumu Uturuki kwa kuwashambulia wanajeshi wake mara kwa mara Karibu na mpaka.

Kinasema kuwa vifaru vya Uturuki vimeshambulia eneo moja linalodhibitiwa na vikosi hivyo karibu na mji wa Jarablus huku gari lake moja likilipuliwa karibu na Kobane.

Uturuki imesema kuwa inachanguza madai hayo.

Imesisitiza kuwa oparesheni yake inayoendelea haiwalenga Wakurdi wa Syria pamoja na kundi la kikurdi la PKK nchini Iraq.

Wakati huohuo waziri mkuu nchini Uturuki Ahmet Davotuglu amepinga kupelekwa kwa wanajeshi wa ardhini ili kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State.

Maafisa wa polisi nchini Uturuki wameendelea kuwakamata wanachama wa kundi la IS na wale wa PKK wanaoshukiwa katika uvamizi wa mapema.