Mnenguaji ahukumiwa Misri

Image caption Mmoja ya wanenguaji nchini Misri

Mnenguaji wa kike nchini Misri amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kuonekana kwenye video yenye utata mtandaoni.

Ametiwa hatiani na mahakama moja nchini humo kwa kosa la kuchochea ufisadi baada ya kuonekana katika video yenye utata katika mtandao.

Reda al - Fouly alitiwa mbaroni mwezi Mei mwaka huu, mara baada ya video hiyo ya miondoko ya Pop kuoneshwa hadharani na baadaye kudhihakiwa kuwa imeenda kinyume na tamaduni za kiarabu.

Muimbaji huyo wa kike alitakiwa kufafanua mavazi -aliyoyava kwenye wimbo unaoitwa Sib Eddi au let it go of my hand.

Mkurugenzi wa video hiyo, Wael Seddiki , aliondoka nchini Misri wakati wimbo huo ulipoanza kupondwa kwenye mitandao ya kijamii.