Putin:Blatter ana haki kupewa tuzo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Urusi Vladimir Putin

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kiongozi wa FIFA,Sepp Blatter ana haki ya kutunukiwa medali ya uongozi bora wa kuliongoza shirikisho la kandanda duniani.

Maafisa kadhaa wa shirikisho hilo bado wapo ndani ya uchunguzi unaofanywa na taifa la marekani kwa tuhuma za rushwa.

Rais Putin ambaye alikuwa kwenye jukwaa moja na Blatter siku ya jumamosi ili kupata fursa ya kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018 kufanyika nchini Urusi.

Raisi huyo alitoa maoni hayo kwenye kituo cha luninga cha uswizi.''siaamini kama Blatter mwenyewe aliusika na ubadhilifu wa fedha kwa rushwa''.

Blatter mwenyewe hakushukiwa lakiniameamua kujiuzuru pale atakapopatikana raisi mwingine wa shirikisho.