Mashambulizi dhidi ya Houthi yasitishwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Yemen

Majeshi ya muungano yakiongozwa na jeshi la Saudi Arabia yamesitisha mashambulizi yake ya angani nchini Yemen, baada ya kuanza muafaka wa amani wa kusitisha mapigano.

Muafaka huo umeafikiwa kati ya majeshi hayo na wapiganaji wa Houthi chini ya Umoja wa mataifa, ili kuyaruhusu mashirika ya utoaji misaada kufikisha chakula na dawa kwa watu wanaothirika na mapigano hayo.

Lakini duru za habari zasema kumekuwa na mashambulizi makali ya roketi kusini mwa Yemen, hata kabla ya kuanza kwa muda huo wa kusitisha mapigano.

Walioshuhudia wanasema kuwa, waasi wa Houthi, waliyashambulia kwa roketi makaazi ya waaribu na mji wa Taiz, mahali ambapo inaaminika kulishuhudiwa mapigano makali katika siku za hivi karibuni.