Je,wajua kufanyakazi usiku kuna athari?

Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Kazi usiku

Kumekuwa na utafiti ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa miongoni mwa watu wanaofanya kazi usiku na jinsi inavyoathiri afya yao vibaya.

Ni swala la kuchemsha bongo kulingana na mwandishi Sarah Montague.

Kwa miaka kadhaa sasa nimekuwa nikiamka usiku ili kwenda kazini, hio ndio gharama ya kufanya kipindi hiki na ni kipindi nafurahia kufanya.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Kazi usiku

Nimekuwa nikijiuliza kama ntaathirika pakubwa kwa siku za baadae.

Je, huenda kuamka kwangu usiku nikiwa sijatosheka usingizi ukawa unaathiri mwili wangu, shida inayoweza kutibiwa na kulala vyema?

Mimi ni mmoja tu wa watu 3.5 milioni nchini Uingereza ambao hufanya kazi kwa zamu wengine wakifanya kazi kwa masaa mengi zaidi na kufanya kazi usiku wote

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Kazi usiku

Na si kwa wale wanaofanya kazi usiku pekee kwani watu zamani walikuwa wanalala kwa saa 8 lakini sasa wengi hulala saa 6 na nusu

Watu wengi hudhania kulala ni starehe.

Kengele yangu ikilia 3.25 asubuhi, mimi hujiambia nitalala zaidi baadae.

Lakini kulala ni swala la umuhimu kama tu kula na kupumua.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Kazi usiku

Huo ni wakati wa akili zetu kufanya kazi kwa yale tumeyafanya katika nyakati za siku nzima na kutengeneza mawazo ya kumbukumbu, huku mwili ukidumishwa.

Tumekuja kugundua kwamba hata iwapo wanaofanya kazi usiku hulala mchana, wao hulala masaa yasiyofaa.

Ili kujua mengi

Sarah Montague anafanya kazi usiku katika BBC redio 4.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Kazi usiku

Imekuwa ikiaminika kuwa mili yetu huenda ikazoeshwa kufanya kazi usiku lakini kutokana na mtaalamu Proff Russel Foster kutoka chuo kikuu cha Oxford, utafiti unaonyesha kuwa mwili huwa hauzoei mabadiliko hayo.

Wanaofanya kazi usiku huenda wakapata magonjwa kama vile ugonjwa wa kisukari aina ya 2, ugonjwa wa moyo na hata saratani.

Wanasayansi wanasema mtu yeyote anayefika kazini mwendo wa saa kumi asubuhi, kama mimi, wana uwezo mdogo wa kutatua maswala sawa tu na mtu aliyekunywa pombe.