Wanaonunua mali kwa pesa chafu UK waonywa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption David Cameron

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, anatarajiwa kulaani matumizi ya pesa chafu kutoka maeno mbali mbali ya dunia zinazotumiwa kununua mali nchini Uingereza .

Katika hotuba anayotarajia kuitoa nchini Singapore muda mfupi ujao , Bwana Cameron anatarajiwa kuahidi kufichua taarifa ya kutumiwa kwa kampuni za kununua mali za kifahari , na kusema kuwa Uingereza haipaswi kuwa mahala pa pesa za wizi .

Zaidi ya mali laki moja ya Uingereza yamesajiliwa kwa majina ya kampuni za kigeni, na zaidi ya robo ya makampuni hayo yako jijini London.