Mwana wa Gaddafi ahukumiwa kifo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mahakama ya libya

Mahakama moja nchini Libya imemuhukumu kumyonga mwana wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Gaddafi,Saif al Islam na wengine wanane kufuatia uhalifu wa kivita uliohusishwa na mapinduzi ya mwaka 2011.

Walikuwa wameshtakiwa pamoja na washirika wengine wa kiongozi huyo aliyeondolewa mamlakani kwa kujaribu kazima maandamano wakati wa mapinduzi hayo.

Saif al Islam hakuwepo mahakamani na alitoa ushahidi wake kupitia teknolojia ya kanda ya video.

Kwa sasa Saif anazuiliwa na kundi moja la waasi la zamani katika mji wa Zintan ambao wamekataa kumuachilia huru.