Obama awaonya viongozi wa Afrika

Haki miliki ya picha epa
Image caption Obama -AU

Rais wa Marekani Barrack Obama,amewasuta viongozi wa Afrika ambao wanaendelea kusalia madarakani hata baada ya katiba kutowaruhusu kuendelea kuwania tena wadhfa wa urais.

Katika hotuba ya kwanza ya rais wa Marekani kwa muungano wa Afrika katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa,amesema kuwa Afrika haitapiga hatua iwapo viongozi wake watakataa kuondoka madarakani baada ya muda wao kuisha.

Amemtaja hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini, ambaye alikaa madarakani kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano na anafahamika pakubwa kote duniani huku akiheshimiwa kama kigogo wa bara Afrika, tofauti na marais wengi wanaoendelea kukwamia madaraka.

Ameongezea kuwa wakati waandishi wanapofungwa huku wanaharakati wakitishwa,demokrasia huwepo tu kwa jina.

Akimnukuu shujaa Nelson Mandela akisema kuwa unapoheshimu uhuru wa wengine watu wote huwa huru.

Amesema kuwa ishara kuu ya maendeleo katika taifa ni vile linavyowachukulia wanawake wake.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Obama

Amewaambia viongozi wa Afrika kwamba maendeleo ya bara hili yanategemea demokrasia,uhuru na haki za kibinaadamu.

Anasema kuwa muda umewadia wa kubadilisha mtizamo wa Afrika kama bara duni lenye kulemewa na umaskini na mizozo.

Aidha amepongeza umoja wa Afrika AU na shirika la Umoja wa mataifa katika mapambano dhidi ya makundi ya wapiganaji wa kiislamu kama vile, Boko Haram kaskazini mwa Nigeria na Al - Shaabab Afrika mashariki.

Amemtaja hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini, ambaye alikaa madarakani kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano na nafahamika pakubwa kote duniani huku akiheshimiwa kama kigogo wa bara Afrika, tofauti na marais wengi wanaoendelea kukwamia madaraka.