Kiongozi wa kundi la Taleban amefariki

Image caption Mullah Omar

Habari kutoka kwa serikali ya Afghanistan zimeiambia BBC kuwa kinara mkuu wa kundi la wapiganaji wa Taliban, Mullah Omar amefariki.

Lakini habari hizo bado hazijathibitishwa rasmi na kundi hilo.

Kwa miezi kadhaa kumekuwepo na tetesi kuhusiana na kifo cha Mullah Omar.

Kifo hicho kimetokea wakati ambapo serikali ya Afghanistan ilikuwa inajiandaa kuanza mashauriano ya amani na kundi hilo la Taliban.

Waandishi wa habari wameitwa na serikali ili kuhudhuria kikao cha wanahabari jijini Kabul, ambao unatazamiwa kufanyika muda mchache ujao.

Taarifa nyingine zinasema kuwa huenda alifariki miaka kadhaa iliyopita.