Uturuki yashambulia kambi za Wakurdi

Haki miliki ya picha na
Image caption Vikosi vya Uturuki katika kizuizi cha barabarani

Serikali ya Uturuki inasema kuwa ndege za kivita zimetekeleza mashambulizi katika kambi za kundi la Kikurdi PKK Kaskazini mwa Iraq na kusini mashariki wa Uturuki.

Ankara imesema kwamba mashambulizi ya PKK nchini Uturuki yamefanya mazungumzo ya amani kutoendelea.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ramani

Waandishi wanasema kuwa mashambulizi ya Uturuki kwa PKK kufikia sasa yamekuwa mabaya zaidi ikilinganishwa na yale ya kundi la Islamic state katika eneo hilo,na hivyobasi kuthibitisha madai kwamba ajenda yao kuu ni kudhoofisha malengo ya kisiasa ya Wakurdi.

Kampeni ya Uturuki dhidi ya makundi yote mawili ilishinikizwa na mlipuaji wa kujitolea muhanga ndani ya Uturuki.