Zimbabwe:Waliomuua simba Cecil kushtakiwa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Cecil

Wanaume wawili wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Zimbabwe baadaye leo wakishtakiwa kwa makosa ya uwindaji , baada ya simba maarufu nchini humo kuuawa na mtalii mmoja raia wa Marekani .

Simba huyo,Cecil,alipigwa risasi nje kidogo ya mbuga ya wanyama ya taifa ya Hwange na Walter Palmer, daktari wa meno na mtu anayependa uwindaji Bwan Palmer -ambaye pia anaweza kukabiliwa na mashtaka , anasema anajuta kwa kumpiga risasi , lakini akasema alidhani alikua katika mawindo halali.

Maandamano juu ya kuuawa kwa simba huyo yamefanyika nje ya makaazi ya bwana Palmer katika jimbo la Minnesota nchini Marekani .