Al Jazeera:Kesi Imeahirishwa tena

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uamuzi wa kesi dhidi ya waandishi wa habari wa shirika la habari la Al-Jazeera nchini Misri umeahirishwa tena.

Uamuzi wa kesi dhidi ya waandishi wa habari wa shirika la habari la Al-Jazeera nchini Misri umeahirishwa tena.

Shirika hilo lilifahamishwa kuwa, Mohamed Fahmy, Baher Mohamed na Peter Greste waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani mwaka uliopita hawataweza kusikizwa leo.

Habari kutoka Cairo zinasema kuwa hukumu ya kesi dhidi ya waandishi tatu wa habari wa Al Jazeera wanaoshtakiwa kwa kulisaidia kundi lililopigwa marufuku la ''The Muslim Brotherhood'' imeahirishwa hadi mwezi ujao.

Mmoja wa waandishi hao , Baher Mohamed, aliambiwa na maafisa wa mahakama kuwa hakuna kesi itakayoendeshwa mahakamani hii leo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Peter Greste,raia wa Australia alirejeshwa kwao

Hii ilikuwa licha ya kuwa wakili wake kupokea taarifa rasmi ya kuthibitisha kuwa kesi hiyo ingesikizwa leo .

Mohamed na wenzake Mohammed Fahmy waliachiliwa kwa dhamana mwezi Februari.

Mwandishi wa tatu wa Al Jazeera ,Peter Greste, ambaye ni raia wa Australia alirejeshwa nyumbani mwezi huo huo na alitarajiwa kuhukimiwa bila kuwepo mahakamani.